Back to top

TANZANIA YAPIGA HATUA HAKI ZA BINADAMU

18 September 2023
Share


Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt.Pindi Chana, amesema Tanzania imeendelea kupiga hatua kubwa, katika maeneo ya uzingatiaji wa haki za binadamu na utoaji wa huduma za msaada wa sheria, mambo yanayochochea uwepo wa amani na maendeleo ya nchi.

Dkt.Pindi Chana amesema hayo, alipokuwa akizindua rasmi kampeni ya msaada wa sheria ya Mama Samia Legal Aid, katika Mkoa wa Simiyu.

Amesema wamejipanga kuhakikisha kampeni hiyo inawafikia Watanzania wote bila gharama wala ubaguzi.

Waziri Chana amewahimiza wazazi na walezi Mkoani Simiyu, kuacha kuwapeleka watoto kwenye kuchunga mifugo, badala yake wawape haki ya elimu kwa kuwapeleka shuleni.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe.Suleiman Zedi amepongeza utekelezaji huo na kuahidi kamati hiyo kutoa ushirikiano.