Back to top

Tanzania yapokea dozi mil.1 ya chanjo UVIKO-19

23 March 2022
Share

Waziri wa Afya, Mh.Ummy Mwalimu kwa niaba ya serikali amepokea dozi milioni moja za chanjo ya Sinovac kutoka serikali ya Uturuki ambazo zitasaidia kuchanja watu 500,000 ambapo mpaka sasa Serikali imepokea jumla ya chanjo ya UVIKO-19 dozi 10,845,774 zikijumuisha (Sinopharm, Janssen, Moderna, Pfizer na Sinovac) ambazo zinatosha kuchanja watu 6,381,327.


Waziri amesema hadi kufikia Machi 21, 2022 jumla ya watu milioni 3,016,551 wamepata chanjo kamili kati ya watu milioni 30,740,928 wenye umri wa miaka 18 na kuendelea ikiwa ni sawa na asilimia 9.81.
.
Hata hivyo, Waziri Ummy amewasisitiza viongozi na watendaji wa ngazi zote kuendelea kutoa ushirikiano ili wananchi waendelee kuhimizwa kupata elimu ya chanjo ili wapate chanjo wajikinge na maambukizi ya UVIKO-19.