Back to top

Tanzania yapokea vifaa Kinga vya Corona kutoka kwa Jack Ma na Alibaba

25 March 2020
Share

Msaada wa vifaa kinga vya kupambana na virusi vya Corona vilivyotolewa na Bilionea wa China Jack Ma na Alibaba Foundation vimeshawasili Tanzania na kupokelewa na serikali.

Vifaa vilivyopokelewa ni Mask, nguo na vifaa vya kupimia Corona pamoja, ambapo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amemshukuru Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ambaye amepewa jukumu la kuvisambaza vifaa hivyo kwenye nchi zote za Afrika.