Back to top

TANZANIA YAPONGEZWA KWA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA AFYA

28 July 2023
Share

Shirika la Afya Duniani (WHO), limeipongeza Tanzania kwa kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya afya, pamoja na kutoa ushirikiano kwa mashirika ya kimataifa hususan Shirika hilo.
.
Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 28, 2023 na Mwakilishi Mkazi wa WHO nchini, Dkt.Charles Sagoe-Moses wakati wa akiwasilisha hati za utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt.Stergomena Tax, katika Ofisi Ndogo za Wizara hiyo zilizopo mkoani Dar es Salaam.
.
Aidha, Dkt.Sagoe-Moses ameongeza kuwa juhudi za Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na magonjwa ya mbalimbali hususan yale ya mlipuko ni nzuri na zinaridhisha, ambapo ametolea mfano namna Tanzania ilivyopambana na homa ya Marburg katika mkoa wa Kagera.