Back to top

Tanzania yaweka msimamo kwa watakaobainika kuwa na Corona.

23 March 2020
Share


Serikali imesema kuanzia leo wasafiri wote watakaongia nchini kutoka kwenye mataifa yaliyoathirika zaidi na ugonjwa wa Corona, watalazimika kufikia sehemu za kujitenga na kukaa huko kwa siku 14 kwa gharama zao wenyewe.

Akililihutubia taifa kwa njia ya Televisheni kutoka Ikulu ya Chamwino Dodoma kuhusu ugonjwa huo Rais John Pombe Magufuli alisema kuna wagonjwa 12 walioambukizwa ugonjwa wa Corona hapa nchini, wakiwemo Watanzania 8.