Back to top

TANZIA: Maalim Seif Sharif Hamad Afariki Dunia hospitali ya Muhimbili.

17 February 2021
Share

Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Mwinyi ametangaza kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad aliyefariki katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Rais Mwinyi ametangaza siku 7 za maombolezo na bendera kupepea nusu mlingoti, huku akisema taifa limepoteza kiongozi mzalendo na shupavu.

Mwinyi amsesema kwamba taarifa zaidi kuhusiana na msiba wa Maalim Seif zitaendelea kutolewa na serikali kwa ushirikiano wa karibu na familia pamoja na chama cha ACT Wazalendo.

Bofya Video Hapa kufahamu zaidi.