Back to top

TARI kuendelea kutekeleza maagizo ya serikali

20 May 2022
Share

Dr.Juliana Mwakasendo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) amemuhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Sara Msafiri kuwa Taasisi hiyo kupitia vituo vyake 17 itaendelea kutekeleza maagizo ya serikali ili kuwaongezea tija wakulima kwa kuhakikisha inabuni mbegu zinazoendana na mabadiriko ya tabia nchi na kuendelea kusambaza teknolojia zilizobuniwa kutoka kwenye maabara na kuwafikia wakulima popote walipo ili walime kibiashara na kuwa na uhakika wa chakula, kipato na kuchangia ukuaji wa uchumi katika nchi.
.
Aidha, Dr. Mwakasendo amesema Taasisi hiyo inatumia njia mbalimbali kusambaza teknolojia zinazobuniwa ikiwemo Siku ya Mkulima, mashamba ya mfano, mafunzo, machapisho mbalimbali, vyombo vya habari (TV na radio), mitandao ya kijamii majukwaa bunifu ya wadau kwenye mnyororo wa thamani, maonesho mbalimbali na tovuti.