Back to top

TARURA Kiteto yaanza kukarabati barabara zilizoharibiwa na mvua.

19 June 2020
Share

Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) wilaya ya Kiteto umeanza kukarabati barabara zilizoharibiwa na mvua ili ziaweze kutumika katika msimu wa huu mavuno kwa kusafirisha mazao kutoka mashambani kwenda kwenye masoko.

Akikagua ukarabati wa barabara hizo Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Bwana Tumaini Magesa amesema ukarabati huo unapaswa kwenda kwa kasi, ili zianze kutumika na wakulima kusafrisha mazao yao na kujipatia kipato.

Meneja wa TARURA wilaya ya Kiteto Bwana Edwin Magari amesema licha ya ukarabati huo kuanza, wakala unakabiliwa na changamoto ya mifugo kuziharibu barabara.

Baadhi ya wakazi wa Kiteto waliozungumza na ITV wameiomba (TARURA) ijenge mifereji mikubwa ya kupitisha maji, ili barabara hizo ziweze kudumu na kuwasaidia wananchi.