Back to top

(TAWA) yaendesha msako kuwasaka Chui wanaoua na kula mifugo Mbinga.

27 October 2018
Share

Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) imeendesha msako mkali wa kuwasaka Chui wanaoleta  hofu na taharuki kwa wananchi wilayani Mbinga  mkoani Ruvuma kwa kuua kondoo 40,mbuzi 22 na ngo'mbe wawili hadi sasa.

Kwa upande wake kaimu  afisa  mtendaji wa kata ya Ruanda Bw.Elgius Ndimbo anawataka wananchi kufungia mifugo yao kwenye mazizi badala ya kuiacha ikizurula ovyo maporini na kwamba kata hiyo imepakana na mapori ya akiba ya Litumbandyosi na Liparamba  ambako chui wanatokea.