Back to top

TBS: MAZIWA YA INFACARE YAMESAJILIWA TANZANIA

15 May 2024
Share

Shirika la Viwango nchini (TBS), limesema maziwa mbadala ya watoto aina ya Infacare 1, 2 na 3 yanayozalishwa na kiwanda cha Sanulac Nutritionals South Africa (Pty) Ltd. cha nchini Afrika Kusini, yamesajiliwa na Shirika hilo, baada ya kuhakiki ubora na usalama wake.
.
TBS imetoa taarifa hiyo ikiwa ni siku chache tu baada ya Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) kutoa taarifa juu ya uwepo wa maziwa hayo yaliyoandikwa "Not for Resale in Tanzania” ambayo yaliingizwa Zanzibar pasipo kufuata utaratibu na hivyo kusitishwa matumizi na kuondolewa katika soko.
.
Shirika hilo limesema Taarifa za bidhaa za Infacare zilizosajiliwa zimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili kwa pamoja kwa mujibu wa Kiwango EAS 4-1:2021 na Kanuni za Usajili wa Bidhaa na Uthibitishaji Ubora wa Shehena [The Standards (Imports Registration and Batch Certification) Regulations, 2021].
.
Aidha, TBS imebainisha kuwa bidhaa zilizosajiliwa hazijaandikwa “Not for Resale in Tanzania" hivyo wananchi wanatakiwa kutoa taarifa kupitia namba 0800110827 endapo watabaini kasoro zozote kwenye taarifa zilizopo kwenye vifungashio vya maziwa mbadala ya watoto.