Back to top

TBS yapiga marufuku uingizwaji bidhaa zisizo na ubora nchini.

30 July 2020
Share

Shirika la Viwango nchini (TBS) limepiga marufuku uingizwaji wa bidhaa za vyakula amabazo hazijathibitishwa na wataalamu wa ubora  kwenye masoko, ili kumlinda mwananchi dhidi ya madhara ya nayotokana na matumizi ya bidhaa zisizo na ubora.

Agizo hilo limetolewa Mkoani Geita na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bw.Hamisi Sudi alipokuwa akizungumza na wawekezaji na wajasiriamaki wa bidhaa za vyakula kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Bw.Fadhili Juma amewataka wananchi kutoa taarifa kwa watu wanaoingiza bidhaa zisizo na ubora na amewataka wawekezaji kutengeneza bidhaa zenye ubora ili kuleta ushindani kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Mkoa wa Geita, Bw.Jafari Donge amesema wameanza mpango maalum kuwawezesha wawekezaji wazawa na wajasiriamali ili watengeneze bidhaa zenye ubora .