Back to top

TCAA kuendelea kusimamia usalama wa usafiri wa anga nchini.

24 August 2019
Share

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Nchini (TCAA ) Bw.Hamza Johari amesema mamlaka hiyo itaendelea kusimamia mifumo ,Sera ,Sheria na kanuni zote zilizopitishwa na shirika la usafiri wa anga ulimwengu katika kuhakikisha kuwa usafiri wa anga nchini unaendelea kuwa salama.

Bwana Hamza anaeleza dhamira hiyo mara baada ya kushuka kutoka kwenye kilele cha mlima Kilimanajaro cha Uhuru walipopanda kupandisha bendera ya shirika la anga ulimwenguni ICAO ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka sabini na tano tangu kuundwa kwa shirika hilo.

Mwaka huu shirika la anga ICAO linatarajia kufanya baraza lake kuu nchini Canada ambapo Bwana Hamza Joharia anasema TCAA itatumia fursa hiyo kuutangaza mlima Kilimanjaro kwa kwa ulimwengu wa wasafiri wa anga.

Safari ya kuipandisha bendera hiyo ya ICAO mlima Kilimanjaro ilifanywa na watu ishirini kutoka TCAA na wadau wengine wa usafiri wa anga ambao kati yao tisa wakiongozwa na mkurugenzi mkuu walifanikiwa kufika kileleni na kuipandisha na kuipeperusha rasmi bendera hiyo.