Back to top

TCB yaagizwa kujenga ghala la kuhifadhia na kuuza kahawa.

03 July 2020
Share

MOSHI KILIMANJARO.

Naibu Waziri wa Kilimo , Mhe.Hussein Bashe ameiagiza Bodi ya Kahawa Tanzania kwa ushirikiano na Benki ya Kilimo Tanzania kujenga nchini China ghala la kuhifadhia na kuuza kahawa iliyosindikwa.

Ametoa agizo hilo alipotembea Bodi ya Kahawa kuona shughuli za uendeshaji wa mnada unavyokuwa katika Soko la Dunia na kuzungumza na wafanyakazi na menejmenti ya bodi hiyo.

Mhe.Bashe amesema kwa kujenga ghala hilo na kuuza kahawa iliyosindikwa katika nchi hizo kutasaidia kupanua wigo wa soko la Kahawa ya Tanzania ambayo inapendwa na mataifa mengi duniani.

Hata hivyo Naibu Waziri wa kilimo ambaye alikuwepo kwa ziara ya siku mbili kuzitembelea taasisi zilizo chini ya wizara yake ameahidi kurejea tena kutokana na muda mfupi aliokuwa nao.