Back to top

Tembo 30 wavamia mashamba na makazi ya watu wilayani Namtumbo.

28 April 2021
Share

Tembo 30 wakiwa katika makundi mawili wamevamia makazi na mashamba ya wananchi na kuharibu ekari zaidi ya 20 za mazao mbalimbali na kuzusha taharuki kubwa kwa wananchi katika kijiji cha Mbimbi wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.
.
ITV imetembelea mashamba yaliyoharibiwa kijijinii hapo katika kata ya Litola ambapo wananchi  wamepatwa na hofu kubwa na kupelekea kushindwa kwenda shambani kufuata chakula  huku wakijipoza kwa kuokota kinyesi cha tembo kinachodaiwa kuwa ni dawa ya magonjwa mbalimbali.
.
Afisa Maliasili wa  wilaya ya Namtumbo Bw.Simbalu Simon  amesema kuwa wamefanikiwa kuwarejesha tembo hao kwenye hifadhi ya Nyerere walikotokea.
.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Bi.Sophia Kizigo amesema kuwa makundi ya tembo yametamalaki wilayani humo ikiwemo kata ya Litola kutokana na wafugaji na wakulima kuharibu ikolojia  ya hifadhi na kusababisha tembo kutoka hifadhini.