Back to top

TET kuwezeshwa kuchapa vitabu nchini.

15 May 2022
Share

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Prof. Adolf Mkenda ameitaka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kuweka mkakati wa ndani ya mwaka mmoja kuhakikisha inapata mashine kubwa ya kuchapa vitabu na kutafuta tenda nafuu ya malighafi ya karatasi ambapo agizo hilo linakuja wakati matumizi ya serikali kwa ajili ya kuchapisha vitabu vya nukta nundu vinavyotumiwa na wanafunzi wasioona na wenye uoni hafifu ikiwa ni Bilioni 15 kwa mwaka.

Prof.Mkenda ametoa maagizo hayo alipofanya ziara ya kutembelea vituo vya kuchapisha vitabu cha Press A Magogoni na Press B kilichopo shule ya Uhuru Mchanganyiko Jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa kiasi hicho kinatokana na malighafi ya karatasi inayotumika kuchapa kununuliwa Dubai na Marekani.