Back to top

Tetemeko la ardhi lapita Dar.

12 August 2020
Share

Tetemeko la ardhi limepiga Dar es salaam majira ya saa  mbili na dakika 13 usiku huu na kuibua mshtuko maeneo mbalimbali.

Mtaalam wa Jiolojia  kutoka Makao Makuu ya Dodoma  Bw. Gabriel  Mbogoni  amesema tetemeko hilo ni la kiwango cha 5.9 cha kipimo cha  ritcher na limetokea  Kusini mashariki mwa Dar es salaam  na Mkuranga upande wa baharini.

Hakuna madhara yaliyoripotiwa  hadi sasa  ingawa maeneo ya Pwani, Morogoro, Arusha na Zanzibar wameripoti tetemeko hilo.