Back to top

Tetemeko la Ardhi laua 2 na kujeruhi 4 Indonesia.

21 November 2022
Share

Tetemeko kubwa la ardhi limetikisa Kisiwa Kikuu cha Java nchini Indonesia na kuharibu majengo kadhaa kisha kupelekea wakaazi wa eneo hilo kuelekea katika mitaa ya mji mkuu kwa usalama. 

Watafiti wa Jiolojia wa Marekani walisema tetemeko hilo la kipimo cha 5.6 siku ya Jumatatu lilitokea katika eneo la Cianjur katika mkoa wa Java Magharibi kwa kina cha kilomita 10.

Kulingana na taarifa ya Shirika la Kitaifa la kukabiliana na Maafa limesema, tetemeko hilo limeua watu 2 na kujeruhi wengine 4 huku majengo kadhaa yakiharibiwa ikiwa ni pamoja na shule moja ya kiislamu, hospitali na vifaa vingine vya umma.

Tetemeko hilo limeua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne, Shirika la Kitaifa la Kukabiliana na Maafa lilisema. Makumi ya majengo yaliharibiwa, ikiwa ni pamoja na shule ya bweni ya Kiislamu, hospitali na vifaa vingine vya umma.