Back to top

TICTS yatakiwa kuimarisha utendaji kazi wake

08 April 2022
Share

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS) kuimarisha utendaji kazi wake ikiwemo kuacha kuchelewesha ushushaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam huku akisisitiza kuwa kampuni hiyo ina paswa kufanya kazi kwa weledi na kupitia mkataba wa utendaji kazi wake ili kuhakikisha inatoa huduma stahili kwa wateja wanaohudumiwa katika bandari hiyo.
.
Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo alipozungumza na Viongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS) na kukagua utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam kufuatia maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan.