
Serikali ya Somalia imepiga marufuku mitandao ya kijamii ya TikTok na Telegram na programu ya kamari ya mtandaoni, ikisema kuwa ilikuwa inatumiwa na "magaidi" kueneza propaganda.
Hatua hiyo inakuja kabla ya awamu ya pili ya mashambulizi ya kijeshi, yanayotarajiwa dhidi ya kundi la wanamgambo wa Kiislamu Al-Shabaab,ambalo limekuwa likiendesha uasi wa umwagaji damu dhidi ya serikali kuu mjini Mogadishu, kwa zaidi ya miaka 15.
Katika taarifa, ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia, iliagiza watoa huduma za intaneti kutekeleza marufuku hiyo kufikia Agosti 24 la sivyo wachukuliwe hatua za kisheria ambazo hazijabainishwa.
