
Watu tisa wameuawa wakati wa mapumziko ya mwisho mwa wiki nchini Guinea, ambapo makomando wenye silaha walivamia gereza, na kumtoa gerezani aliyekuwa dikteta Moussa Dadis Camara, maafisa wamethibitisha tukio hilo leo Jumatatu.
Watu waliokuwa na silaha nzito walivamia gereza, katika mji mkuu wa Conakry mapema Jumamosi, wakamchukua Camara na maafisa wengine wawili wa zamani, ambao walikuwa wakishtakiwa pamoja naye kwa mauaji ya 2009 wakati wa urais wake.
Haikuwa wazi kama Camara, alitoroka kwa hiari yake mwenyewe au au amechukuliwa kwa nguvu katika uvamizi huo, ambao jeshi lilielezea tukio hilo kama jaribio la "kuhujumu" mageuzi ya serikali.
