Back to top

TMA yasema mvua za masika zinaendelea, yatoa tahadhari.

20 April 2018
Share

Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA imesema mvua za masika  zitaendelea kuwepo hadi mwezi wa tano huku wakazi wa mabondeni wakiendelea kutahadharishwa.

Kauli hiyo imezungumzwa na meneja wa uendeshaji wa vituo vya hali ya hewa, Bi. Hellen Msemwa, ambapo  amesema maeneo machache sana yanatarajiwa kupata vipindi vifupi vya mvua kubwa.