Back to top

TMA yasema tetemeko la Ritcher 5.9 halikusababisha TSUNAMI.

13 August 2020
Share

Kufuatia tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha Ritcher 5.9 katika eneo la kusini Mashariki mwa mkoa wa Pwani katika bahari ya Hindi lililotokea Agosti 12, 2020, Mamlaka ya hali ya hewa Tanazania (TMA), imesema hakuna tishio la Tsunami kutokana na tetemeko hilo.

TMA imelazimika kutoa taarifa hiyo bada ya kuifanyia uchambuzi katika kituo chake cha tahadhari ya Tsunami ili kuona na kujiridhisha kwamba kuna uwezekano wowote wa tetemeko hilo kusababisha mawimbi ya Tsunami baharini.

"Tetemeko hilo halikuwa na nguvu kubwa na hakuna maporomoko ya ardhi yaliyojitokeza baharini ambayo yangeweza kuzalisha Tsunami"-Imeeleza taarifa hiyo.

TMA imewatoa hofu watumiaji wa eneo la bahari pamoja na wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyokaribu na bahari ya Hindi kutokuwa na hofu na kuendelea na shughuli zao kwa kuzingatia taarifa zinazo tolewa na mamlaka hiyo.

Hata hivyo TMA imesema kutokana na tetemeko hilo hakuna athari iliyojitokeza au inayotarajiwa kujitokeza katika mifumo ya hali ya hewa ya bahari.

Aidha TMA imeongeza kuwa inaendelea kufuatilia mifumo ya hali ya hewa baharini na kutoa taarifa endapo kutajitokeza mwenendo wa matetemeko katika eneo la bahari.

NB:Tetemeko hilo lili pita Jijini Dar es Salaam, ikiwemo Mikocheni, Temeke, Ilala, Tabata na Ubungo mwendo wa saa 2:14 Usiku, lakini Pia Arusha, Morogoro, Lindi, Zanzibar na Mobassa Kenya nk, ni maeneo yanayotajwa kupitiwa na tetemeko hilo.