Back to top

TMA yatahadharisha juu ya ujio wa mvua kubwa.

13 February 2020
Share

Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetangaza kuwapo kwa  mvua kubwa katika maeneo mbalimbali nchini kuanzia wiki ya pili ya mwezi wa tatu hadi wiki ya pili ya mwezi watano.

Taarifa hiyo imetolewa  leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya mamlaka hiyo.

Aidha kuhusu athari za mvua hizo Dk. Kijazi amesema mafuriko yanatarajiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hivyo tahadhari zinapaswa kuchukuliwa.

Kuhusu tahadhari ya kuwapo wadudu aina ya Nzige, ambao wameingia nchi za jirani, Dk.Kijazi alizitaka mamlaka mbalimbali kutumia taarifa hiyo kuchukua tahadhari kutoka mielekeo ya upepo.