Back to top

TMA yatoa utabiri wa mvua za msimu.

21 October 2020
Share

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA)  imetoa Utabiri wa mwelekeo wa mvua za msimu kwa kipindi cha kuanzia mwezi Novemba mwaka huu hadi mwezi Aprili mwakani ambapo imesema mvua zitaanza kunyesha wiki ya pili ya mwezi Novemba na  Utabiri unaonesha uwepo wa mvua za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya nchi.


Akitoa utabiri huo  Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa TMA  Dk Agness Kijazi amesema viashiria vinaonesha kuwa mvua itanyesha kwa kiwango kizuri .