Back to top

TMDA yatoa elimu ya matumizi sahihi ya dawa kwa wanafunzi Ruvuma.

24 June 2020
Share

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imetoa elimu ya matumizi sahihi  ya dawa ikiwemo sanitizer na barakoa kwa wanafunzi  mkoani Ruvuma ili kuwakinga na madhara yatokanayo na matumizi  yasiyo sahihi ya dawa.

Elimu hiyo imetolewa kwa baadhi ya shule wilayani Songea ikiwemo shule ya sekondari ya Londoni ambapo wanafunzi wametakiwa kuwa makini na matumizi sahihi ya dawa.

Kwa upande wao walimu na wanafunzi  wamesema wamenufaika mno na elimu iliyotolewa na kwamba elimu hiyo inahitajika sana kwa kipindi hiki ambacho kumekuwepo na matumizi holela ya dawa.