
Afisa Uendeshaji wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) Mahama Kadikilo, amesema kuelekea msimu wa mbaazi wa mwaka 2024/25 wanunuzi wapatao 20 wameshajisajili kwa kwenye mfumo wa manunuzi kwa ajili ya kununua zao hilo.
Kadikilo amebainisha hayo, kwenye kikao cha stakabadhi ghalani kilicholenga kutathimini mauzo ya zao la ufuta pamoja na maandalizi ya msimu wa mbaazi, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara.
"Niseme tu kwamba matajiri wa kununua mbaazi wanajitokeza Kila siku hata nilipokuwa hapa ndani kwenye kikao cha mkuu wa mkoa wa Mtwara nilikuwa nasajili wanunuzi. Kwa hiyo nilikuwa nainama hapo wananiuliza maswali tufanye hivi tuweke hela shilingi ngapi nawatumia miongozo nawaelekeza" alisema Mahama Kadikilo,Afisa uendeshaji wa soko la bidhaa Tanzania (TMX).
Kadhalika Kadikilo amesema tayari mpaka sasa umefanyika mnada mmoja huko mkoani Manyara ambapo bei ya kilogramu moja imeuzwa kwa bei ya shilingi 2,151 na Bei ya chini shilingi 2,090.
