Back to top

TNMC: WAUGUZI NA WAKUNGA FUATENI MAADILI.

04 August 2024
Share

Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC) limesema ni vyema jamii ikafahamu haki na wajibu wa mteja au mgonjwa pindi anapofika kupewa huduma za Afya katika kituo cha kutolea huduma ikiwemo kupatiwa taarifa za mgonjwa na matibabu yake, Kupatiwa matibabu bila kukemewa, kukaripiwa au kufedheheshwa,Kupata huduma kwa wakati, kutegemea aina ya huduma, Kuwa na hiyari kupata taarifa zako za kiafya.

Hayo yamebainishwa na Afisa Uhusiano  Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC) Ezekiel Nyalusi, Jijini Dodoma katika maonesho ya Nanenane.

Ndugu Nyalusi ameainisha haki zingine kuwa ni kupata huduma stahiki kwa makundi maalumu kama vile, Walemavu, Wazee, Wajawazito, Watoto wa chini ya miaka mitano na wenye magonjwa sugu, kulalamika au kutoa mrejesho wa huduma uliyopatiwa, Kufuata kanuni na taratibu za kituo husika, Kuwaheshimu watoa huduma ikiwa ni pamoja na kutumia lugha Safi, Kumueleza muhudumu wa afya taarifa zote ambazo zitamuwezesha kutoa tiba sahihi ikiwa ni pamoja na kumpa rekodi za matibabu ya awali .

Kwa Upande wake Bi. Irene Chilewa ambaye ni Kaimu mkuu kitengo cha Udhibiti Ubora TNMC,  amewataka wauguzi na wakunga kufuata Kanuni za Maadili ya Uuguzi na Ukunga Tanzania  ikiwemo ya kutimiza wajibu  na kuwa tayari  kuwajibika kwa matendo yao.

TNMC imeshiriki Maadhimisho ya maonesho ya kitaifa ya Nanenane kwa muda wote wa siku nane ikitoa huduma mbalimbali za Baraza, kama vile Uhuishaji wa leseni, sajili na utoaji wa elimu ya sheria na maadili kwa wauguzi na wakunga na kutoa elimu ya haki ya mteja akiwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya.