Back to top

TNMC: WAUGUZI NA WAKUNGA ZINGATIENI UTU

05 February 2024
Share

Wauguzi na Wakunga wametakiwa kuendelea kutoa Huduma kwa kuzingatia Maadili, Sheria, kanuni na taratibu ili jamii iweze kupata Huduma bora na Salama.
.
Hayo yamesemwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC), wakati wakitoa mafunzo ya maadili na sheria ya Uuguzi na Ukunga kwa wauguzi na wakunga katika Halmashauri zote Mkoa wa Geita, ambapo pia wamekumbushwa kutanguliza utu katika utoaji huduma.
.
Akitoa mafunzo hayo Msajili wa Baraza hilo, Bi.Agnes Mtawa, amebainisha kuwa takribani 60% hadi 80% ya watoa huduma za Afya nchini, ni Wauguzi na Wakunga, hivyo ni vyema wakapata mafunzo hayo ili kuendelea kuboresha zaidi Huduma za afya nchini.