
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Abdallah Ulega amesema kuwa Serikali itaendelea kuziondoa tozo zote zinazoonekana kukwamisha shughuli za Uvuvi ili wavuvi waweze kufanya shughuli zao vizuri kukuza kipato chao na Taifa kwa ujumla,.Ametoa kauli hiyo jijini Mwanza akiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi walipotembelea Mwalo wa Kirumba.
