Back to top

TRA Kigoma kudhibiti wafanyabiashara wa vitenge wanaokwepa kodi.

27 February 2021
Share

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kigoma imeanza kuchukua hatua dhidi ya ukwepaji kodi unaofanywa na waagizaji wa vitenge kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Burundi ambao baadhi yao wamekuwa wakitumia njia za panya kuingiza bidhaa hiyo nchini ili kukwepa kodi.

Meneja Makusanyo na Madeni wa mamlaka hiyo mkoani Kigoma Jeremiah Maunde amesema mamlaka imebaini ukwepaji wa kodi unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wa vitenge na kwamba itaanzisha oparesheni na kuziba mianya yote kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, ili kuhakikisha  wafanyabiashara hao wanalipa kodi ipasavyo wanapoingiza bidhaa na wanatoa stakabadhi wanapouza hapa nchini.

Kwa upande wao, wafanyabiashara hao wamesema wanakabiliwa na changamoto kadhaa kutoka nchi hizo zikiwa ni pamoja na kutopewa stakabadhi za  malipo ya kod, hivyo wameiomba Mamlaka ya Mapato ikutane nao ili kuzijadili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.