Back to top

TRA YATAKIWA KUANGALIA MSAMAHA WA KODI YA MAJENGO

01 June 2022
Share

Waziri wa Fedha na Mipango Dr.Mwigulu Nchemba ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania kuangalia utekelezaji wa agizo la msamaha wa kodi ya majengo kwa kuwasamehe wanaotakiwa kusamehewa kodi hiyo.

Waziri Nchemba amesema hayo Bungeni mkoani Dodoma wakati akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa Wizara hizo kuhusiana na msamaha wa kodi ya majengo kwa baadhi ya watu ama taasisi.

Aidha Waziri Nchemba amesema Serikali imekuwa ikitoa msamaha wa kodi ya majengo kwa watu ambao wamekuwa wakifuata taratibu zilizowekwa na kuwataka wenye kuhitaji msamaha huo wafuate taratibu hizo.

Bunge linaendelea na vikao vyake mkoani Dodoma, ambapo leo hii Wizara ya Nishati inawasilisha makadirio ya mapato na matumizi yake kwa mwaka wa fedha 2022/23.