Back to top

TRAKOMA tishio kwa wananchi wa Namtumbo na Tunduru.

07 December 2019
Share

Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Sight Savers Tanzania wamezindua mpango wa upimaji wa ugonjwa wa macho wa vikope (Trakoma) katika wilaya za Namtumbo na Tunduru mkoani Ruvuma, kutokana na wananchi wa maeneo hayo hususani vijijini kutajwa kuathirika zaidi na maambukizi ya ugonjwa huo.

Namtumbo na Tunduru ndio wilaya ambazo zinatajwa kuathirika zaidi na ugonjwa huo ambapo kwa sasa kupitia mpango huo sasa utawafuata wananchi vijijini nyumba kwa nyumba kuwapima macho na kuwatibu.

Ugojwa wa macho wa vikope au Trakoma unaambukizwa kwa inzi, Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Bi. Sophia Kizigo anasisitiza usafi katika maeneo ya vyoo huku baadhi ya wananchi wakishukuru mpango huo na kwamba utaleta tija kubwa katika ujenzi wa taifa.