Back to top

Treni yaua wafanyakazi 5 washirika la reli Tanzania.

23 March 2020
Share


Wafanyakazi watano wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) wamefariki dinia katika ajali ya Treni ya uokoaji kugongana na Kiberenge katikia eneo lililopo kati ya Stesheni ya Mwakinyumbi na Gendagenda katikareli inayotoka Ruvu Junction mpaka Mkuranzi Junction jana.

Taarifa ya shirika hilo imesema ajali hiyo imehusisha wafanyakazi sita ambao wanne kati yao walifariki dunia katika eneo la ajali na majeruhi wawili  walifikihswa katika hospitali ya wilaya ya Korogwe, Magunga ambako mmoja alifariki dunia baadaye.

Waliofariki dunia wametajwa kuwa Ramadhan Gumbo, Fabiola Moshi, Joseph Komba, Philbert Kajuna na George Urio.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe Amen.