Back to top

TRENI ZILIZOCHONGOKA (EMU) ZAWASILI NCHINI

03 April 2024
Share

Shirika la Reli Tanzania (TRC), limesema, seti ya kwanza ya treni ya kisasa ya Electric Multiple Unit (EMU), vichwa vitano vya umeme na mabehewa matatu ya abiria yamewasili katika bandari ya Dar es Salaam.
.
Shirika hilo limetoa taarifa hiyo kupitia mitandao yake kijamii ambapo limeeleza kuwa Serikali ilifanya manunuzi ya seti 10 za treni za EMU kutoka kwa watengenezaji kampuni ya Hyundai Rotem ya nchini Korea Kusini, ambapo treni hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 589 na kutembea kwa kasi ya kilomita 160 kwa saa, huku ikiwa imeundwa kwa teknolojia ya kisasa ambayo inamuwezesha abiria kupata hudma mbalimbali ikiwemo Wi-Fi, mifumo ubaridi (AC) na kamera za usalama.
.
Aidha, Shirika hilo limesema, maendeleo ya mradi wa reli ya kisasa ya SGR, awamu ya kwanza yamefikia 98.90% kwa kipande cha Dar es salaam - Morogoro chenye urefu wa kilometa 300, kipande cha Morogoro - Makutupora 96.51%, kipande cha Makutupora - Tabora 13.98%, kipande cha Tabora - Isaka 5.44% na kipande cha Mwanza - Isaka 54.01%.