
Waziri wa Elimu, Prof.Adolf Mkenda amesema serikali itatumia Shilingi Trilioni 1.15 kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa Elfu-12, vifaa vya kujifunzia pamoja na kuwajengea uwezo walimu wa shule za msingi.
Akizungumza katika uzinduzi wa Programu ya Boost, Prof.Mkenda amesema programu hiyo inayolenga kuboresha mazingira ya ufundishaji na kujifunza, kuboresha miundombinu ya shule na kuimarisha uwiano wa uandikishaji wa watoto katika elimu ya awali.
Profesa Mkenda amesema mradi huo utatekelezwa kwa Dola za Marekani Milioni 500 ambazo ni sawa na Shilingi Ttrilioni 1.15 ambapo vyumba vya madarasa Elfu-tatu vitajengwa kila mwaka hadi kufikia vyumba vya madarasa Elfu-12 itakapofika mwaka 2026.
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.David Silinde ameipongeza serikali kwa kudhamiria kuboresha sekta ya elimu kupitia mradi huo ambao unatokana na fedha za mkopo wenye riba nafuu kutoka Benki ya Dunia.
