Back to top

Trump 'agoma; kupunguza ushuru wa forodha kwa China.

09 November 2019
Share

Rais Donald Trump wa Marekani amesema hajakubali kupunguza ushuru wa forodha uliowekwa na nchi yake kwa bidhaa za China.

Akizungumza na waandishi wa habari Rais Trump amesema kuwa China inataka kupunguziwa ushuru wa forodha lakini hajakubaliana juu ya suala lolote.

Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China hivi karibuni amesema nchi hizo mbili zimekubaliana kupunguziana ushuru wa forodha kwa awamu.

Serikali za China na Marekani zimekuwa zikifanya kazi kuandaa mkutano kati ya Rais Trump na Rais Xi Jinping wa China ili wasaini makubaliano ya kibiashara ya awali.

China inaitaka Marekani ipunguze ushuru wa forodha likiwa kama sharti la awali kabla ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Pande hizo mbili zimewekaeana mfululizo wa nyongeza ya ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Marekani inadhamiria kusubiri na kuona ni kwa kiasi gani China ipo tayari kushughulikia masuala muhimu, likiwemo lile la hakimiliki za ubunifu.