Back to top

Trump aifuta ziara yake nchini Denmark. ataja sababu.

21 August 2019
Share

Rais wa Marekani Donald Trump amefutilia mbali ziara yake rasmi nchini Denmark baada ya waziri mkuu wa taifa hilo kusema kwamba Greenland haitauziwa Marekani.

Trump alitarajiwa kuzuru taifa hilo Septemba 2 kufuatia mwaliko wa malkia wa taifa hilo Margethe II na wiki iliyopita alipendekeza kwamba Marekani ilikuwa na hamu kukinunua kisiwa cha Greenland , Jimbo la Denmark linalojitawala.

Waziri mkuu wa Denmark Mette Frederiksen alitaja mpango huo kwamba ni upuzi na kusema kwamba alitumai bwana Trump hakulichukulia swala hilo na uzito mkubwa.

Akitangaza kuvunja safari yake bwana Trump alituma ujumbe wa Twitter akisema Denmark ni taifa maalum lenye watu wazuri sana lakini kutokana na matamshi ya waziri mkuu Mette Frederiksen kwamba hatakuwa na hamu ya kuzumngumzia ununuzi wa Greenland, nitaahirisha mkutano wangu uliopangwa wiki mbili zijazo kwa muda mwengine.

Greenland ndio kisiwa kikubwa zaidi duniani baada ya Australia ambayo inajulikana kama bara ambapo Maafisa katika kisiwa hicho cha Greenland wamesisitiza kwamba kisiwa hicho hakiko katika soko.