Back to top

Trump asalimu amri, akubali ushindi wa Joe Biden.

08 January 2021
Share


Rais wa Marekani anayemaliza muda wake Bwana Donald Trump ameukubali ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi uliofanyika Novemba Tatu 2020.

Hata hivyo, katika hotuba yake kwa njia ya Twitter, amesisitiza umuhimu wa kurekebisha sheria za uchaguzi za nchi hiyo ili kuthibitisha utambulisho na ustahiki wa wapiga kura wote na kuhakikisha imani na ujasiri katika chaguzi zote zijazo.

Amesema baada ya bunge kuthibitisha matokeo na serikali mpya inatarajiwa kuingia madarakani tarehe 20 mwezi huu, mtazamo wake umebadilika na atahakikisha kuwa makabidhiano ya madaraka yatafanyika kwa mujibu wa sheria ili kulinda heshima ya nchi.

Amelaani vurugu zilizotokea katika jengo la bunge kufuatia uvamizi uliofanywa na wafuasi wa chama chake cha Republican na kuahidi kuwa waliohusika watachukuliwa hatua za kisheria.