Back to top

Trump atoa siku 30 kwa shirika la afya duniani kabla hajabadili uamuzi

19 May 2020
Share

Rais Donald Trump wa Marekani amelipa Shirika la Afya Duniani siku thelathini kutekeleza maboresho aliyopendekeza, kabla nchi yake haijaacha kulichangia au kujiondoa uanachama.

Marekani ilisitisha michango yake katika shirika hilo katikati ya mwezi uliopita na kulishutumu kwa kuwa karibu zaidi na China kwa madai kuwa haikutoa taarifa mapema kuhusu virusi vya Corona ili vidhibitiwe.

Kupitia mtandao wa Twitter, Rais Trump amemkumbusha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus kuhusu  barua alizomwandikia kumtaka afanye maboresho katika utendaji wa shirika ambayo kama yasipofanyika Marekani itasitisha kulichangia.

Rais Trump ameonya kuwa kama hayo anayotaka yafanyike hayafanyiki, Marekani inaweza kujiondoa kutoka shirika hilo, licha ya kutochangia.