Back to top

Trump awaacha njia panda maafisa wake wa afya.

29 July 2020
Share

Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine tena ametetea matumizi ya hydroxychloroquine kupambana na virusi vya corona na kudai kuwa dawa hiyo ya kutibu malaria ilikataliwa kutibu Covid- 19 kwa kuwa tu yeye ndiye aliyeipendekeza.

Kitendo hicho alichokifanya Rais Trump kimewachanganya na kuwaacha njia panda maafisa wake wa afya.

Kauli yake imekuja baada ya mtandao wa Twitter kumfungia mtoto wa Trump mkubwa kwa kitendo cha kuchapisha taarifa kuhusu kutumia hydroxychloroquine.

Hakuna ushahidi wowote mpaka sasa kuwa dawa hiyo inaweza kupambana na virusi vya corona na wadhibiti wa dawa wanatahadharisha kuwa inaweza kusababisha matatizo ya moyo.