Back to top

Trump kutangaza hali ya hatari muda wowte kuanzia sasa na Mexico.

15 February 2019
Share

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kutangaza hali ya hatari muda wowote kuanzia sasa kuhusiana na eneo la mpaka katika nchi hiyo na Mexico.

Hali hiyo inatokana na bunge la Congress kukataa kuidhinisha fedha ambazo Rais Trump alizitaka ili aweze kujenga ukuta wa kuzitenganisha nchi hizo kama njia za kuzuia uhamiaji haramu na uingiaji wa dawa za kulevya nchini Marekani.

Kutokana na sheria za Marekani pindi Rais anapotangaza hali ya hatari anaruhusiwa kuchukua mabilioni ya Dola na kuzitumia katika jambo analotaka bila kupatwa vikwazo vya kisheria.
Tangu aingie madarakani Rais Trump amekuwa akitaka ujenzi wa ukuta huo.