Back to top

Tshisekedi atangaza baraza jipya la Mawaziri DRC.

26 August 2019
Share

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DR) Félix Tshisekedi ametangaza baraza jipya la Mawaziri, ambapo katika baraza hilo wanawake wamepewa asilimia kumi na saba na wanaume asilimia 83, baraza ambalo limesubiriwa kwa muda wa miezi 7 tangu achaguliwe kuwa rais wa nchi hiyo.

Mnamo Julai mwaka huu Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila walikubaliana kuunda serikali ya muungano.

Walikubali kuunda serikali itakayo kuwa na mawaziri 66.

Kama walivyo kubaliana, chama cha rais huyo wa zamani sasa kimepata wizara 43, na kile cha rais Félix Tshisekedi kimejinyakulia wizara 23.

Maswali yaliulizwa wakati huo huku kukiwa na madai kwamba bwana Tshisekedi alifanya makubaliano ya kugawana mamlaka na bwana Kabila kabla ya uchaguzi huo.

Mashauriano yamekuwa yakiendelea kati ya vyama vyao na na pande hizo mbili zilieleza kwamba mashauriano hayo yatapokamilika serikali itatangazwa.