Back to top

Tuhuma za wizi wa mabati 1,172 Kilosa, DED Gairo asimamishwa kazi.

10 September 2021
Share

Waziri wa TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Wilaya ya Gairo Bw. Asajile Lucas Mwambambale ili kwenda kujibu tuhuma za wizi wa mabati 1,172 uliotokea Agosti 17, 2021 kwenye Bohari ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.
.
Aidha, Waziri Ummy amemuagiza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI kupeleka timu huru ya kuchunguza kwa kina suala la aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo huku akiwakumbusha watumishi wote wa Sekritarieti za Mikoa na Mamlaka za serikali za mitaa kufanya kazi kwa weledi.