Back to top

Tuhumiwa maarufu wa utekaji na ubakaji akamatwa Morogoro.

26 March 2018
Share

Jeshi la polisi mkoani Morogoro linawashikilia watuhumiwa watano kwa makosa tofauti akiwemo mtuhumiwa sugu anayedaiwa kujihusisha na matukio ya utekaji  watu na kuwabaka kisha kuwapiga picha anazotumia kiwashawishi kutoa fedha ili asizisambaze kwenye mitandao ya kijamii.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrch Matei amemtaja mtuhumiwa sugu wa ubakaji  kuwa ni Mabula Mabula maarufu kama SIX (28) mkazi wa mji mpya katika Manispaa ya Morogoro ambaye inadaiwa amekuwa akijifanya askari polisi ama dereva wa pikipiki  na kuondoka na watu kisha kuwakaba na kuwaingilia kinyume na maumbile na kupiga picha za utupu  halafu hulazimisha atumiwe fedha ili asisambaze picha hizo, ambapo mtuhumiwa huyo akazungumza nia ya kufanya hivyo.

Watuhumiwa wengine watatu wanadaiwa kujihusisha na matukio  ya utapeli kwa njia ya mtandao.

Jeshi la polisi likatoa wito kwa wananchi waliofanyiwa vitendo hivyo kujitokeza polisi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.