
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt.Said Ally Mohamed, amesema jumla ya wanafunzi 1,397,370 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi unaotarajiwa kufanyika kesho, Septemba 13 na 14 nchini kote ambapo amewataka watu wote wanaohusika na mitihani hiyo kuzingatia sheria na kujiepusha na aina zote za udanganyifu.
.
Katibu huyo ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari, ambapo amebainisha kuwa wanaamini wanafunzi hao wameandaliwa vyema katika kipindi chote cha miaka saba, hivyo watakaobainika kufanya udanganyifu watachukuliwa hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na kuwafutia matokeo.
