Back to top

Tukio la ardhi kutitia Songea laleta hofu na taharuki kwa wananchi

11 May 2020
Share

Wananchi wanaoishi jirani na eneo ambalo ekari tano za  ardhi zimetitia mita tano kwenda chini katika kijiji cha Lugagara wilayani Songea mkoani Ruvuma wameshikwa na hofu na taharuki kutokana na tukio hilo.
 
 
Wananchi hao katika kitongoji cha Namasatu kulikotitia ardhi wanasema hofu yao inakuja kutokana na maeneo hayo kuwa ya kilimo na makazi na hivyo ikiwa eneo lingine lenye watu na makazi likakatitia yanaweza kutokea maafa.
 
Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Pololet Mgema ametembelea eneo la tukio na kutoa wito kwa wananchi kuwa makini wanapofanya shughuli zao na watafanya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo kujua limetokana na nini.
 
Mwenyekiti wa kijiji cha  Lugagara Bw.Daniel Mwinuka amemshukuru mkuu wa wilaya kwa kuwatembelea na  kuwatoa hofu na kwamba watachukua tahadhari kwenye shughuli zao.