
Mkazi wa kijiji cha Somanga wilayani Kilwa, mkoani Lindi, Laila ally Mtondwe, miaka 18 amejinyonga kwa kujitundika kwenye dari ya nyumba wanapoishi na bibi yake kwa kutumia mtandio na kupelekea kifo chake.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa lindi Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Mtatiro Kitinkwi, amesema tukio hilo lilitokea tarehe 9/6/2022 majira ya saa tatu asubuhi huko kijiji cha Somanga Kaskazini.
Kamanda Kitinkwi amesema sababu za kujinyonga kwake bado hazijafahamika na mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi katika Kituo cha afya Somanga na kugundulika kuwa sababu za kifo chake ni kukosa hewa, na mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Jeshi la Polisi mkoa wa Lindi linaendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha kifo chake.
