
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta. TULIA ACKSON amesema ipo haja kwa Serikali kuhakikisha kauli yake ya kuwachukulia hatua Wakurugenzi wa halmashauri ambao hawatengi fedha kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi vijana na akinamama.
Naibu Spika amesema hayo bungeni Mjini Dodoma baada ya Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI - Mhe shimiwa JOSEPH KAKUNDA kusema kuwa Serikali itaanza kuwachukulia hatua wakurugenzi ambao hawatekelezi hilo.
Awali bungeni hapo wabunge sita kwa nyakati tofauti, waliohoji sababu za fedha hizo kutotengwa na baadhi ya halmashauri na kuwafanya vijana na akinamama kukosa haki zao.
Pia bungeni hapo Serikali ilishauriwa kuangalia uwezekano wa kuwakopesha watu wenye ulemavu kama ambavyo imetenga kwa ajili ya akinamana na vijana nchini.