
Inadaiwa kuwa kampuni ya Twitter imetishia kuishtaki kampuni ya Meta, Baada ya Meta kuzindua mtandao wake mpya wa 'Threads' ambao umefanikiwa kufikisha zaidi ya watumiaji milioni 30, ndani ya saa 24, duniani kote, kwa madai kuwa Meta imeiba siri za biashara za Twitter, kwa hoja kuwa, iliajiri makumi ya wafanyakazi wa zamani wa Twitter ambao walijua siri hizo.
.
Ikumbukwe kuwa Meta ilitangaza kuzindua mtandao huo jana Alhamis Julai 06, 2023, ambao sifa zake nyingi zinafanana na mtandao Twitter, kwa lengo la kuleta ushindani kwa Twitter, ambao hivi karibuni umekuwa ukitambulisha sera mpya ambazo nyingi zimekuwa zikilalamikiwa na watumiaji wa mtandao huo.
.
Kufuatia mvutano huo, mmiliki wa mtandao wa Twitter Bw.Elon Musk ameibuka kupitia, mtandao huo na kuchapisha ujumbe kuwa "Ushindani ni sawa, lakini sio kwa udanganyifu".
.
Hata hivyo, Kampuni ya Meta haijakaa kimya juu ya tuhuma hizo ambapo, Msemaji wa kampuni hiyo Bw.Andy Stone, kupitia 'Threads' amejibu kuwa kwenye timu ya Threads hakuna mfanyakazi aliyewahi kufanya kazi Twitter.
