Back to top

TWITTER KUTUMIA NEMBO YA 'X' BADALA YA NDEGE

23 July 2023
Share

Mmiliki wa mtandao wa Twitter, Elon Musk, amesema wanapanga kubadilisha nembo ya Mtandao huo kutoka kwenye ndege wa bluu, kuwa herufi 'X', kuashiria mageuzi makubwa yaliyofanyika tangu alipoununua mtandao huo.
.
Ikumbukwe kuwa Bilionea huyo anayemiliki makampuni mbalimbali ikiwemo SpaceX, mnamo oktoba 2022, alituma ujumbe kupitia Twitter, kuwa kununua mtandao huo ni kuongeza kasi ya kuunda 'X'.
.
Musk ametajwa kuwa na historia ndefu na herufi hiyo, kwani mnamo mwaka 1999 alianzisha kampuni ya huduma za kifedha iliyojulikana X.com, ambayo kwa sasa inajulikana kama PayPal.